County Updates, Diocese of Marsabit, Editorial, Local Bulletins, National News

ASILIMIA 95 YA MADARASA YA GREDI YA 9 KATIKA SHULE ZA MSINGI SEKONDARI JSS KAUNTI YA MARSABIT YAMEKAMILIKA. – ASEMA MKURUGENZI WA ELIMU KATIKA KAUNTI YA MARSABIT PETER MAGIRI.

Na Isaac Waihenya & Abdilaziz Abdi,

Angalau asilimia 95 ya madarasa ya gredi ya 9 katika shule za msingi sekondari JSS kaunti ya Marsabit yamekamilika

Haya yamewekwa wazi na mkurugenzi wa elimu katika kaunti ya Marsabit Peter Magiri.

Akizungumza na shajara ya Radio Jangwani ofisini mwake Magiri amesema kuwa ni asilimia tano pekee ndio imesalia huku zoezi hilo likitarajiwa kukamilika kabla ya mwisho wa mwezi ujao wa Oktoba.

Magiri amekariri kuwa walimu wakuu wa shule za msingi sekondari JSS hapa jimboni pia wametaja kwamba wamejiandaa kikamilifu kwa majaribio ya wanafunzi wa gredi ya sita KPSEA.

Kuhusiana na mtihani wa kidato cha nne aidha Magiri amesema kuwa aslimia kubwa ya shule za upili zimekamilisha silabasi huku zikiwa tayari kwa mtihani wa kitaifa KCSE.

Kadhalika mkuu huyo wa elimu jimboni ametaja kwamba idara hiyo iko macho zaidi kuzuia wizi wa mitahini ya kitaifa KCSE huku wasimamizi wa mitihani hiyo wakihamishwa kutoka vituo vya mitihani kila baada ya wiki moja.

Subscribe to eNewsletter