Afueni kwa wanafunzi 132 wa shule ya upili ya Goro Rukesa baada ya KNEC kuachilia matokeo ya mitihani yao….
January 21, 2025
Mila potovu imetajwa kama sababu kuu ya visa vya ukeketaji kuendelea kuongezeka katika kaunti ya Marsabit.
Kwa mujibu wa mwanaharakati wa kutetea haki za binandamu kutoka eneo la Log Logo Eunice Basele, aliyeongea na meza ya habari ya Radio Jangwani kwa njia ya kipekee, ni kuwa bado jamii imeshikilia mila ambazo zinawataka wasichana kukeketwa Jambo linalolemaza vita dhidi ya kero hilo.
Bi. Basele ametaja kwamba ipo mbinu mbadala ya kuwahitimisha wasichana kupitia mafunzo na wala sio lazima wakeketwa ili kuvuka kutoka daraja moja hadi jingine.
Aidha Bi. Basele ameweka wazi kuwa idadi kubwa ya wasichana ambao hawajakeketwa wanapitia unyanyapa kutoka kwa jamii huku akirai jamii kuwakumbatia badala ya kuwadhihaki.
Hata hivyo mtetezi huyu wa haki za binadamu amependekeza mafunzo zaidi kwa wavulana ili kuhakikisha kwamba vita dhidi ya ukeketaji vinafaulu hapa jimboni Marsabit.