MILA NA TAMADUNI ZATAJWA KUWA KIKWAZO KWA WANAWAKE KUFANYA MAZOEZI YA MWILI MARSABIT.
November 20, 2024
MWAKILISHI wadi wa Obbu, Halkano Rare amekariri haja ya idara ya usalama hapa Marsabit kusaidia kuondolewa kwa wafugaji kutoka eneobunge la Eldas, Wajir ambao wanaendelea kulisha mifugo yao katika wadi ya Obbu, Sololo kaunti hii ya Marsabit.
Rare ameambia Radio Jangwani kuwa licha ya ofisi yake kutoa ombi kwa idara ya usalama kuwafurusha wafugaji hao bado wanaendelea kuwamalizia malisho ambayo walikuwa wanahifadhi kwa ajili ya kipindi cha kiangazi kijacho.
MCA Rare akizungumza Jumamosi iliyopita katika eneo la Dambala Fachana aliitaka serikali kuwaondoa wafugaji hao kwani wamejihami kwa bunduki suala wanalosema ni hatari kwa usalama wao raia wa Marsabit. Amerejea wito huo tena kwa idara ya usalama.
Naibu kamishna wa Sololo Edward Goko hata hivyo ameahidi kufuatilia swala hilo kwa karibu akishirikiana na DCC wa Eldas. Ameahidi kuwa watafanya mkutano kati ya wakaazi wa upande wa Eldas na wale kutoka upande wa Marsabit.
Amesema kuwa machifu wa pande zote mbili waliongoza mkutano wiki jana japo haikuzaa matunda. Anasema kuwa mkutano mwingine wa pande hizo mbili hutafanywa siku ya Jumamosi wikii hii.
Kuhusu suala la njaa DCC Goko amesema kuwa serikali inazidi kuwapa chakula cha msaada wakaazi wa Sololo huku wakisubiri chakula Zaidi.