Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
Asilimia 90 ya watoto ambao wapo chini ya umri wa mwaka mmoja wako katika hatari ya kukumbwa na hali ya kifo cha ghafla (SIDS) iwapo wazazi hawatamakinika katika malezi.
Haya ni kwa mujibu wa afisa wa kliniki ya Watoto katika hospitali ya rufaa ya Marsabit Galm Wako.
Akizungumza na idhaa hii, Galm ameelezea kuwa japo haijabainika kamili kinachosababisha hali hiyo, ni jukumu la mzazi kuwa karibu na mtoto wake pamoja na kubadili mienendo inayohatarisha maisha ya watoto.
Galm ameelezea kuwa visa vya Vifo vya ghafla kwa watoto wachanga (SIDS)havijaweza kubainika katika kaunti ya Marsabit kutokana na watu kutoripoti visa vya hivi katika hospitali ama zahanati na badala yake wanaamua kuzika watoto pindi tu wanapofariki.
Galm hata hivyo Galm amesema kuwa visa vya mimba za mapema pia huchangia hali hii ya watoto kufariki ghafla kwa ajili ya ukosefu wa malezi Bora.
Afisa huyu ametoa wito kwa akimama wajawazito kuzingatia kliniki zao, ili kuepuka visa hivi na hata baada ya kujifungua wawe wafuate maelezo ya kuboresha afya na malezi bora ya watoto.