Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
Wahalifu wa wizi wa mifugo kutoka kaunti jirani zinazopakana na kaunti ya Marsabit wameonywa vikali dhidi ya kutekeleza mashambulizi hapa jimboni Marsabit.
Ni onyo ambalo limetolewa na kamishna wa kaunti ya Marsabit James Kamau.
Onyo hili linajiri kufuatia jaribio la wizi wa mifugo wiki jana katika eneo la Ell Nedeni mjini Marsabit ambapo watu waliotajwa kutoka kaunti jirani na ambao walikuwa wamejihami kwa bunduki walivamia wafugaji katika jaribio la kuiba mbuzi zaidi ya 100 ambapo mhalifu moja aliuawa na maafisa wa polisi.
Aidha machifu kutoka maeneo ya mpakani ikiwemo Laisamis, Songa, Kituruni, Shurr, Jaldesa na maeneo mengine yaliyo mipakani wameagizwa kuwa makini ili kuwatambua watu wanaohofIwa kuwa wahalifu wa wizi wa mifugo.
Kamishna Kamau amezungumza haya wakati wa maadhimisho ya siku ya mazingira, hafla iliyoandaliwa katika eneo la kambi nyoka kaunti ndogo ya Turbi kaunti ya Marsabit.
Kamishna kamau pia amewataka wafugaji jimboni kuchukua tahadhari wakati wa malisho.
Wakaazi jimboni nao wakitakiwa kutoa taarifa muhimu kwa vyombo vya usalama ili kufanikisha vita dhidi ya wizi wa mifugo.
Kadhalika amesema kuwa idara ya usalama jimboni inaendelea kurejesha usalama kat