Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
Watu wanne wameshtakiwa katika mahakama ya Marsabit kwa kosa la ulanguzi wa bangi leo Ijumaa.
Wanne hao wanaojuimusha Anthony Mbae, Boniface Mwenda, Benjamin Muiruri na Danson Mureithi walikamatwa wakisafirisha kilo 10 za bangi zenye thamani ya shilingi 160,000 katika makutano ya Burgabo katika barabara ya Moyale kuelekea Marsabit saa nne usiku wa kuamkia Ijumaa.
Kulingana na kamanda wa polisi kaunti ya Marsabit Leonard Kimaiyo ni kuwa wanne hao walikuwa wakisafirisha bangi hiyo kutumia ya gari aina ya Toyota Fielder lenye usajili ya nambari KDK 975B.
Baada ya kusimamishwa na maafisa wa polisi vifurushi 12 vya bangi yenye uzani wa kilo 10 vilipatikana.
Mbele ya hakimu mkuu mwandamizi Christine Wekesa wanne hao wamekanusha mashtaka dhidi yao.
Wameachiliwa kwa dhamana ya shilingi 200,000 au shilingi 100,000 pesa taslim.
Kesi hiyo itatajwa tena tarehe 8 mwezi huu wa Octoba.