Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
Na JB Nateleng,
Naibu kamishna wa Marsabit ya Kati David Saruni ametoa wito kwa jamii ya Marsabit kutowaficha watu wanaoishi na ulemavu na badala yake kuwalinda na kuwatunza kama watu wengine.
Saruni amesema kuwa wakazi wa Marsabit wanafaa kuasi Mila potovu inayowadunisha watu wanaoishi na ulemavu kwa sababu imepitwa na wakati.
Ameeleza kuwa serekali kuu inawajali watu wanaoishi na ulemavu hata kupitia bima mpya ya afya SHIF
Afisa mkuu katika idara ya tamaduni,jinsia na huduma za jamii katika kaunti ya Marsabit Anna Maria Deng’e amewataka akinamama kuwapeleka wanao katika zahanati iliyopo karibu iwapo watajifungua mtoto aliye na kasoro ili kuzuia ulemavu.