Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
Na Isaac Waihenya,
Wito umetolewa kwa wakazi wa Marsabit kuasi vitendo ambavyo vinapotosha maadili na kupelekea ongezeko la idadi ya vijana wanaotumia mihadarati.
Kwa mujibu wa mwanaharakati anayepambana na matumizi ya mihadarati na dawa za kulevya hapa jimboni Fredrick Ochieng, ni kuwa vijana wa kizazi hiki wanajifunza mambo mengi kupitia vitendo akitolea mfano wa mitandao ya kijamii ya TikTok ambapo baadhi ya mafunzo yanapotosha vijana.
Akizungumza na idhaa hii kwa njia ya kipekee, Ochieng amewataka washikadau mbalimbali pamoja na walezi kuweza kuangazia suala hili kwani ndio chanzo kikuu cha kuenea kwa matumizi na ulanguzi wa mihadarati jimboni.
Amewataka wazazi kuweza kuwachunga wanawao wakiwa nyumbani na pia kudhibiti matumizi ya mitandao kwa kuwapa majukumu ya nyumbani.
Ochieng amesema kuwa matumizi ya mihadarati huenda yakaathiri Elimu hapa jimboni kutokana na kuwa idadi kubwa ya wanaotumia mihadarati ni wanafunzi.
IMwanaharakati huyu ametoa wito kwa serekali kuu kuhamisha polisi ambao wamekaa eneo moja kwa zaidi ya miaka mitatu akisema kuwa hili itasaidia katika kudhibiti uuzaji na matumizi ya mihadarati katika kaunti ya Marsabit.