Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
Na Isaac Waihenya
Wito umezidi kutolewa kwa wakaazi mjini Marsabit kujitokeza kutoa damu ili kusaidia walionamahitaji ya damu hapa jimboni Marsabit.
Kwa mujibu wa afisa kwenye idara ya kutoa damu katika hospitali ya rufaa ya Marsabit Daniel Ngacha ni kuwa utoaji damu una manufaa mengi kwa mwili wa binadamu na hivyo wanaMarsabit hawafai kuhofia zoezi hilo.
Akizungumza na Shajara ya Radio Jangwani katika uwanja wa michezo wa Marsabit kabla ya zoezi la maonyesho ya biashara yanayoandaliwa katika uga huo hapa mjini Marsabit, Ngacha aliwataka wote watakaohudhuria hafla hiyo na wanauwezo wa kutoa damu kutembelea hema ya idara hiyo ili kufanya vile.
Aidha Ngacha aliwarai wanaMarsabit kutokuwa na wasiwasi kuwa damu yao huenda ikauzwa au kutumika vibaya na badala yake wakumbatie zoezi la kutoa damu kila baada ya miezi mitatu ili kuokoa maisha ya wengi wanaohitaji damu hiyo.