Levaquin: Comprehensive Guide on Usage, Benefits, and Safety
December 20, 2024
Na Samuel Kosgei,
Wazee kutoka upande wa Merile wa Marsabit na Sereolipi upande wa Samburu kwa pamoja wamelaani vijana na wahalifu wanaowahangaisha wapita njia na wanabiashara wa mifugo katika Barbara kuu ya Isiolo – Moyale.
Wazee hao waliopatana katika eneo la Milima Mitatu upande wa Samburu Mashariki wameapa kuwa wakati wa visa vya uhalifu na uporaji Barabarani umeisha kwani hawatawaficha au kuwasaza tena wakora.
Wakiongozwa na mzee Salim Nesashore ambaye ni mwenyekiti wa amani Samburu mashariki wanasema kuwa ukosefu wa usalama barabarani mwaka jana umekuwa kero kuu kwa wasafiri hivyo kuna haja ya wazee kulaani vijana wanaharibu usalama njiani.
Kauli yake imeungwa mkono na mwenyekiti wa Amani Laisamis Peter Galwarse anayesema kuwa wizi wa mifugo barabarani imeumiza biashara ya mifugo katika soko la merile na hivyo basi kuwa kuzima kitega uchumi cha wananchi marsabit kwa ujumla.
Naibu kamishna wa kaunti ndogo ya laisamis Wycliffe Langat amesema kuwa serikali imeimarisha doria katika barabara hiyo kwa kutuma polisi kulinda wasafari na mali yao. Amewataka wananchi kutokuwa na wasiwasi kwani wazee pia wameahidi kushirikiana na serikali.
Mwakilishi wadi wa waso kaunti ya Samburu Kelvin Lemantan amewataka wazee hao kuwalaani wazee wengine wanaosaidia vijana kuiba kwa kutumia hirizi.
MCA wa Laisamis/Merile Daniel Burcha amekashifu vijana wanaohangaisha wasafiri na wanabiashara akisema kuwa uchumi wa Merile imeshuka chini kutokana na wizi hiyvo kuna hatari ya sokola mifugo kufungwa iwapo wezi hawatakomeshwa.