Serikali ya kaunti ya Marsabit yaondolea wazazi wasiwasi kuhusu hatima ya ufadhili wa elimu.
January 21, 2025
Na Isaac Waihenya
Vijana wa klabu ya Soka ya Samba Boyz hapa mjini Marsabit wameirai jamii ya Marsabit pamoja na vilabu vingine kuwa katika mstari wa mbele kutoa damu ili kuokoa maisha ya wale wanaohitaji damu hiyo.
Wakiongozwa na nahodha wao Siba Burcha vijana hao wametaja kwamba wamechukua jukumu la kuhamasisha jamii kuhusiana na umuhimu wa kutoa damu ili kusaidia kuokoa maisha haswa ya akina mama na ambao hukumbwa na tatizo la ukosefu wa damu hususan wakati wa kujifungua.
Burcha ametoa wito kwa jamii pia kuendeleza jukumu hilo katika maeneo mengine ya jimbo hili.
Aidha Burcha amekariri hoja ya jamii kupuzilia mbali dhana potovu kuhusu kutoa damu huku akitoa wito kwa viongozi wa jimbo la Marsabit pia kuwa mfano mwema kwa jamii kwa kujitokeza na kutoa damu pia.
Afisa mkuu mtendaji katika hospitali ya rufaa ya Marsabit Kussu Abduba ameisifia hatua hiyo huku akivitaka pia vilabu vingine kuiga mfano huo.