MILA NA TAMADUNI ZATAJWA KUWA KIKWAZO KWA WANAWAKE KUFANYA MAZOEZI YA MWILI MARSABIT.
November 20, 2024
Na Samuel Kosgei
WAZIRI wa Ardhi na Ukuaji wa Miji kaunti ya Marsabit Amina Challa Abdi ametoa onyo kwa wanyakuzi wa ardhi ya umma kuwa chuma chao ki motoni kwani wizara yake inaweka mikakati mwafaka ya kuhakikisha kuwa ardhi zote zilizo mikononi mwa wanyakuzi zinarejeshwa kwa serikali ya jimbo.
Akizungumza na kituo hiki katika majengo ya bunge la Marsabit Amina alisema kuwa wizara yake haitaruhusu tena ardhi za umma kuzidi kuwa chini ya wanyakuzi ambao hakuwataja.
Kwenye suala la baadhi ya vyumba vya soko kuu mjini Marsabit kutomilikiwa na wafanyabiashara licha ya kupewa anasema kuwa wanaokataa kuzitumia wamepewa notisi ili kurejesha umiliki wa vyumba hivyo.
Kwenye mchakato wa serikali ya kaunti kupanga kuwapa wananchi vyeti vya kumiliki ardhi waziri amesema kuwa shughuli hiyo ya kutoa vyeti itakamilika katika kipindi hiki cha kifedha mwaka 2023/24.
Sasa alitoa wito kwa wananchi kuunga mkono zoezi hilo kwa kuwapa ushirikiano masoroveya wa kaunti wanaoendeleza zoezi hilo nzima.