Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
Na Isaac Waihenya na Samuel Kosgei
Mwanaume mmoja wa miaka 50 ameuawa na wezi wa mifugo katika eneo la Shrine eneobunge la Saku kaunti hii ya Marsabit.
Kulingana na kamanda wa polisi kaunti ndogo ya Marsabit ya Kati Johnston Wachira ni kuwa mbuzi 100 waliibwa na majambazi hao waliojihami kwa bunduki.
Ameongoza kuwa maafisa wa polisi walifanikiwa kurejesha ngo’mbe 135 waliokuwa wameibiwa kwenye kisa hicho cha Ijumaa mchana.
Makabiliano kati ya Wezi hao wa Mifugo na maafisa wa KWS baada ya kisa hicho,yalipekelea msafara wa waziri wa Maji Alice Wahome aliyekuwa kwenye ziara ya kukagua bakuli ya maji katika msitu wa Marsabit kusitishwa kwa muda wa dakika 10.
Mkasa huo ulijiri muda mfupi baada ya naibu gavana wa kaunti ya Marsabit, Solomon Gubo Riwe kutoa wito kwa serekali ya kitaifa kuwapa bunduki maafisa wa akiba KPR katika kaunti ya Marsabit ili kutatua kero la ukosefu wa usalama jimboni.
Riwe ambaye amemrai waziri wa maji aliyezuru kaunti ya Marsabit kukagua miradi ya Maji Alice Wahome kufikisha ujumbe kwa Rais William Ruto pamoja waziri wa usalama wa ndani Kithure Kindiki kurakisha swala hilo ili kufikisha kikomo ukosefu wa usalama sawa na wizi wa mifugo.
Mkasa huu unajiri wiki moja baada ya watu 8 kuuawa kwa kupigwa risasi na wezi wa mifugo katika eneo la Kargi wiki jana.