Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
Na Isaac Waihenya
Mgawanyiko kati ya wanachama wa kundi la Saku Forum for Disabled wanaomiliki duka la maji lililopo karibu na shule ya msingi ya St Theresa hapa mjini Marsabit umezidi baada ya kundi hilo kumuondoa Waqo Kumbi kama wawakilishi wa kundi hilo kwenye kamati ya idara ya maji jimboni na nafasi yake kuchuliwa na Wato Tadicha.
Kwa mujibu wa naibu mwenyekiti wa kundi hilo Julius Kinoti ni kwamba, Kumbi pamoja na wengine wawili ambao ni katibu wa kundi hilo Mohamed Galgalo mwanachama Madina Daud watachukuliwa hatua za kinidhamu.
Akizungumza na vyombo vya habari Kinoti alisema kuwa watatu hao wanatakiwa kuomba msamaha kwa uongozi wa idara ya maji kwa kile ambacho alikitaja kwamba ni kuikosea idara hiyo heshima.
Kinoti alitoa wito kwa wanachama kuzika tofauti zao na kuungana kwa faida ya chama hicho.
Aidha waliahidi kushirikiana na MARSWASCO ili kuhakikisha kwamba wanaendeleza shughuli zao za kusimamia kuuza maji na kujipatia mapato yao ya kila siku.