Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
Na Isaac Waihenya
Kampuni ya maji katika kaunti ya Marsabit MARWASCO imewataka wakaazi wa mji wa Marsabit kuwa na subira inapoendeleza zoezi la kurekebisha mifereji ya maji iliyoharibiwa wakati wa ujenzi wa barabara katika maeneo mbalimbali hapa mjini.
Akizungumza wakati wa mkao na wateja wa MARWASCO uliolenga kusikiliza lalama za wateja hao kutoka mjini wa Marsabit na vyunga vyake, mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo Sora Katelo alisema kuwa kwa sasa kampuni hiyo inazidi kuimarisha huduma zake kwa wananchi ili kuhakikisha kwamba wanapata maji kwa wakati.
Katelo alipendekeza kutumiwa kwa upepo kuzalisha nguvu za umeme hapa mjini ili kutatua swala la ukosefu wa maji ambalo muda mwingi husababishwa na ukosefu wa umeme.
Vilevile Katelo aliitaja hoja ya mji wa Marsabit haswa idara muhimu kama ya maji kuunganishwa na umeme kutoka kampuni ya Lake Turkana Wind Power ili kufikisha kikomo kero la kupotea mara kwa mara kwa uguvu za umeme.
Aidha kampuni hiyo iliahidi kuangazia upya ada zinazotozwa wananchi ili kuhakikisha kwamba haziwafinyi mno hususan kipindi hichi ambacho gharama ya maisha imepanda.
Malalamishi yaliyoibuliwa na wananchi ni ikiwemo, ada ya juu wanayotozwa, ukosefu wa maji sawa na urekebishaji wa mifereji ya maji, maswala na ambayo kampuni ya MARWASCO imeahidi kuyashugulikia haraka iwezekanavyo.