Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
Na Samuel Kosgei,
MKURUGENZI wa idara kilimo kaunti ya Marsabit Julius Gitu amesema kuwa suluhu pekee ya kuweza kuzalisha chakula cha kulisha wananchi wa marsabit siku za usoni ni kuweka mikakati ya kuchimba mabwawa makubwa ili kuyateka maji ya mvua.
Anasema mara kwa mara maji mengi yamekuwa yakipotea pindi mvua chache zinaponyesha suala analodai halingefaa kamwe.
Akizungumza na radio jangwani ofisini, Gitu amesema kuwa maji yanayopotea bure hapa jimboni na yale yanayotoka sehemu za juu za Ethiopia zikikusanywa vyema kwenye mabwawa yanaweza kusaidia mifugo na ktk suala la kilimo cha chakula.
Aidha amesema iwapo maji yaliyo chini ya ardhi yanaweza kutunzwa na kuhifadhiwa vyema basi pana uwezekano mkubwa wa kupatikana kwa maji ya kutosha ardhini.
Ameongeza kuwa maji ya visima yatakauka kutokana na kutokuwepo na mikakati mzuri wa kuyatunza maji yaliyo ardhini hivyo kusababisha ardhi kukauka.