JAMII YA MARSABIT YATAKIWA KUJITOKEZA KUPIMWA UGONJWA WA MENINGITIS ILI KUPATA MATIBABU MAPEMA.
November 15, 2024
Na Isaac Waihenya,
Gavana wa Marsabit Mohamud Ali, amewateua maafisa wakuu 24 kushikilia idara mbalimbali katika serekali yake.
Ishirini na nne hao wameteuliwa kutoka kwa orodha ya watu 101 walioitwa kuhojiwa.
Kwenye taarifa iliyosomwa na katibu wa kaunti Ibrahim Sora ni kuwa idadi hiyo ni tano zaidi ikilinganishwa na 19 zilizokuwemo katika awamu ya kwanza ya Gavana Mohamud Ali.
Idara ambazo zimeongezwa ni ikiwemo idara ya afya ya umaa,Teknologia, idara ya Mali asili, idara ya kukabiliana na majanga pamoja na ile ya Ukusanyaji wa Fedha.
Baadhi ya walioteuliwa ni akiwemo aliyekuwa mkurugezi katika idara ya jinsia Anamaria Qalla Denge atakayeshikilia idara ya kazi ya Umma, aliyekuwa afisa wa utawala katika kaunti ndogo ya North Horr, Roba Qotto atakayeshikilia idara ya Utumishi wa Umma, Orge Guyo aliyekuwa mkurukenzi katika wizara ya utawala hapa jimboni Marsabit ambaye sasa atashikilia idara ya Usalama wa Chakula,pamoja na aliyekuwa Naibu wa katibu wa kaunti ya Marsabit Wolde Weisa.
Wengine ni akiwemo Mohamed Tache wa ICT,Tache Elema wa mawasiliano, Alamin Adan atakayeshikilia idara ya afya, Roba Galma idara ya maji,Abdullahi Sheikh akishikilia idara ya mazingira na mabadiliko ya tabia nchi, Guyo Ali idara ya utalii, Arero Halkano idara ya mifugo pamoja na Mahad Mohamed Diba atakayeshikilia idara ya biashara.
Bwana Boru Duba Dulacha sasa ndie afisa mkuu katika idara ya fedha, Ahmed Intallo ikishikilia idara ya uchumi na mipango ya Bajeti, Qabale Adhi akishilia idara ya elimu, Adan Ali Osman akiteuliwa kushikilia idara ya vijana na michezo huku Bi Samuela Lolokuru akishikilia idara ya jinsia.
Wengine na pamoja na Omar Boko Mohamed, Roba Galma Halakhe, Bi. Pauline Marheni,Galm Guyo Rogicha, Kazali Abdirizaq Bulle, Guyatu Wakala, Bi. Kula Phabbi pamoja na Rikoi Hitler atakayeshikilia idara ya uchukuzi na barabara.
Majina ya 24 hao yatawasilishwa katika bunge la kaunti ya Marsabit kuweza kupigwa msasa na kisha kulishwa kiapo kuhudumu iwapo wataidhinishwa na Ma MCAs.