Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
Na Isaac Waihenya,
Diba Matacho mwanafunzi mwenye umri wa miaka 22 ambaye aliyekuwa amelazwa katika hospitali ya Rufaa kwa muda wa miaka sita amepata alama ya B- kwenye matokeo ya mtihani wa kitaifa yaliyotangazwa hii leo.
Akizungumza na idhaa hii kwa njia ya kipekee Matacho aliyeufanyia mtihani wake wa kitaifa KCSE katika hospitali ya rufaa ya Marsabit ametaja kufurahishwa na matokeo hayo japo alikuwa analenga zaidi ya hapo.
Aidha Diba amewashukuru wote waliosimama naye hadi kufanikisha elimu yake ya kidato cha nne.
Machacho ambaye ndoto yake ni kuwa mhasibu sasa anatoa wito kwa wahisani kuingilia kati ili kuhakikisha kwamba anaeleza elimu yake ya Chuo kikuu.
Kwa upande wake Mwalimu Fauzia Liban anayefunza katika shule ya Marsabit mixed na ambaye ndie aliyekuwa mwalimu wa Diba, amemtaja kama mwanafunzi mtiifu na mwenye nidhafu ya juu huku akikosa kuficha furaha yake kutokana na ufanisi wa mwanafunzi wake Diba Matacho.