Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
Na John Bosco Nateleng
Askofu wa Jimbo hili askofu Peter Kihara amewashauri wanafunzi dhidi ya kujihusisha na wizi wa mitihani.
Akihutubu katika shule ya wasichana ya Bishop Cavallera huko Karare wakati wa hafla ya kuwazawadi wanafunzi waliofanya vyema katika mtihani wa KCSE mwaka jana, askofu Kihara alisema kwamba ni sharti mwanafunzi ajivunie matokeo ambayo amepata mwenyewe kwa jasho lake pasi kuiba mtihani.
Askofu Kihara aidha aliwahimiza wanafunzi kutia bidii masomoni badala ya kujihudisha na visa hivyo vya wizi wa mitihani kwa maana wazazi na walezi wa wanafunzi wengi huangaika kuhakikisha wanao wamelipiwa karo.
Kadhalika Askofu Kihara aliwapa changamoto wazazi kutokata tamaa kulipia wanao karo akitaja kanisa lipo katika mstari wa mbele kuhakikisha ya kwamba hakuna mwanafunzi anafukuzwa shuleni kwa sababu ya kutolipa karo.
Wakati uo huo kiongozi huyo aliwashukuru wafadhili waliosaidia shule ya upili ya Cavallera kupata visima vya maji na mabweni hivyo kuiwezesha shule hiyo kuwavutia wanafunzi wengi.