JAMII YA MARSABIT YATAKIWA KUJITOKEZA KUPIMWA UGONJWA WA MENINGITIS ILI KUPATA MATIBABU MAPEMA.
November 15, 2024
Na Isaac Waihenya,
Takriban watahiniwa elfu 13,405 watanatarajiwa kukalia mitihani ya kitaifa ya Gredi ya 6 KPSEA na darasa la nane KCPE katika kaunti ya Marsabit.
Kwa mujibu wa mkurungenzi wa elimu katika kaunti ya Marsabit Titus Mbatha ni kuwa watahiniwa hao wamejitayarisha kikamilifu kwa ajili ya mitihani hiyo inayotarajiwakuongoa nanga jumatatu juma lijalo huku watahiniwa 7,089 wakikalia mtihani wa Gredi ya 6 ambao ni wa kwanza tangu kuanza kwa mtaala mpya wa CBC nchini.
Akizungumza ofisini mwake,Mbatha ametaja kwamba mikakati yote imeimarishwa ili kuhakikisha kwamba mitihani hiyo inaendelea kwa njia inayostahili huku idadi ya wasichana wanaokalia mitihani hiyo ikionekana kuongezeka ikilinganishwa na miaka ya hapo awali.
Mkuu huyo wa elimu jimboni ametaja biashara ya Bodaboda kama sababu kuu inayopelekea kupungua kwa idadi ya wavulana shuleni haswa baada ya darasa la saba.
Aidha amewataka wazazi jimboni kuwapa wanao haki ya elimu kwani elimu ndio pekee inayoweza kubadili maisha ya WanaMarsabit.