Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
Na Samuel Kosgei,
Mbunge wa Laisamis Joseph Lekuton amepongeza serikali ya kitaifa kwa kuchukua hatua ya haraka na kutuma askari wa kitengo kurejesha amani kwa kasi (RDU) katika lokesheni ya Kambinye eneobunge la Laisamis.
Akizungumza alipowatambulisha askari hao katika Manyatta hiyo ya Kambinye, Lekuton amesema ujio wa askari hao wa RDU ni ishara kuwa serikali imejitolea kupambana na ukosefu wa usalama.
Aidha amewasihi wakaazi wa eneo lake na majirani wao kuishi kwa Amani na utulivu kwa manufaa ya ustawi.
Wakaazi wa eneo hilo wameishukuru serikali pia kwa kusikia kilio chao na kuleta usaidizi wa haraka kwani tayari watu walikuwa wamehama eneo hilo kwa hofu ya kuvamiwa zaidi.
Hatua hiyo ya askari kutumwa eneo hilo inajiri siku kadhaa baada ya watu watatu kuuawa katika visa tofauti Kambinye na shegel wiki Jana.
Amekariri kuwa waziri wa usalama Prof Kithure Kindiki anatariajiwa kuzuri Marsabit hivi karibuni