County Updates, Diocese of Marsabit, Local Bulletins

Kaunti ya Marsabit ina vituo 105 ambavyo havina mtandao wa 3G.

Picha;Hisani.

Na Isaac Waihenya.

Eneo Bunge la North Horr ndilo eneo ambalo limeadhirika zaidi katika kaunti ya Marsabit kwenye orodha ya maeneo yaliyoratibishwa na tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC kuwa hayana mtandao wa 3G.

Kwa ujumla kaunti ya Marsabit ina vituo 105 ambavyo havina mtandao wa 3G kati ya vituo 384 vya kupigia kura.

Kwa mujibu wa IEBC ni kuwa vituo 55 vya kupigia kura katika eneo bunge la North Horr havina mtandao wa 3G, eneo bunge la Laisamis nalo likiwa na vituo 27 vya kupigia kura ambavyo havina mtandao huo.

Katika eneo bunge la Moyale, vituo 22 vya kupigia kura havina mtandao wa 3G huku kituo kimoja pekee cha kupigia kura kikiwa hakina mtandao huo katika eneo bunge la Saku.

IEBC kupitia mwenyekiti wake Wafula Chebukati imetaja kuwa itatumia mitambo ya Setelaiti kuweza kupeperusha matokeo haswa katika maeneo na ambayo hayana mtandao wa 3G nchini.

Subscribe to eNewsletter