Jimbo katoliki la Marsabit laadhimisha miaka 60 ya kueneza Injili.
November 23, 2024
By Samuel Kosgei,
WAWAKILISHI Wadi wa kaunti ya Marsabit wameteta sababu zao kupitisha mswada wa kubadilisha katiba mwaka wa 2020 wakidai kuwa ni mswada mzuri kwa wakaazi wa marsabit ikizingatiwa kuwa kaunti nyingi imechangamkia mchakao huo wa BBI.
Wakizungumza nje ya bunge lao MCAs hao wakiongozwa na kiongozi wa wengi Alkano Konso na kiongozi wa wachache Buke Diba wamekariri kuwa wao kama wawakilishi wadi hawana vurugu yoyote bungeni hivyo hawakuona haja ya kulumbana au kupinga.
Diba ambaye pia ni mwakilishi wadi wa maikono ametahadharisha wananchi kutohusisha BBI na siasa za Tangatanga Na Kieleweke akisema kuna haja ya wananchi kuelemishwa Zaidi kuhusu manufaa ya BBI.
Mcas akina mama nao wameonesha kuridhishwa na uamuzi wa bunge hilo wakisema kuwa BBI itaipa nguvu na uwezo akina mama ikizingatiwa na katiba ya sasa. MCA mteule Sadia Araru ametetea hatua yao suala lilioungwa mkono na mwakilishi anayesimamia walemavu Kizito Konchora Abduba