Padre Francisco (Frank) Terragni kupumzishwa hiyo kesho Alhamisi….
January 22, 2025
Na Emmanuel Amalo,
Watoto watatu wamefikishwa katika hospitali ya rufaa ya Marsabit baada ya kupigwa risasi usiku wa kuamkia leo baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana.
Akidhibitisha kisa hicho afisa mkuu wa hospitali ya rufaa ya Marsabit Liban Wako amesema kwamba kwa sasa watatu hao wanauguza majeraha ya risasi ila bado wanaendelea kupokea matibabu.
Haya yanajiri tu baada ya kisa cha jana ambapo watu sita waliaga dunia huku wengine wakiachwa na majeraha baada ya lori aina ya canter kushambuliwa na wasiojulikana katika eneo la Bank Quotters barabara ya Marsabit kuelekea Badassa.