Jimbo katoliki la Marsabit laadhimisha miaka 60 ya kueneza Injili.
November 23, 2024
By Adano Sharawe,
Wasomi wa Jamii ya Borana kutoka Kaunti ya Marsabit na Isiolo wametoa wito kwa Rais Uhuru Kenyatta kuingilia kati na kumaliza hali ya utovu wa usalama katika eneo la Kaskazini ambao wanasema imechochewa na migogoro juu ya mipaka na rasilimali mbalimbali.
Wakihutubia wanahabari jijini Nairobi, wasomi hao wakiongozwa na mwenyekiti wao Suleiman Jillo pia wanadai kumekuwa na ulegevu kwa upande wa serikali katika kutatua mizozo baina ya kijamii ambayo inaendelea kuathiri utoaji wa huduma katika eneo hili.
Jillo anaitaka serikali kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya viongozi ambao anadai wanafadhili mapigano ambayo yamesababisha vifo vya raia na uharibifu wa mali.
Kwa upande wake Mohammed Duba amewalimbikizia lawama maafisa wa usalama kwa kukosa kuwajibika vilivyo na kusababisha mavamizi kuzidi kuripotiwa katika eneo hili.
Wasomi hao wanarejelea matukio ya visa vya mauaji, uvamizi na wizi wa mifugo uliofanyika wiki jana katika eneo la Halakha Yahya na Turbi ambapo watu wawili waliuawa kwenye matukio tofauti huku mifugo Zaidi ya 300 wakiibiwa.