IDARA YA ELIMU KATIKA KAUNTI YA MARSABIT YAWEKA MIKAKATI KABAMBE KUZUIA VISA VYA UCHOMAJI WA SHULE KUTOKEA HAPA JIMBONI.
September 12, 2024
Na Mark Dida
Watahiniwa 197 wa KCSE mwaka 2020 wamejizolea alama ya kuwawezesha kujiunga na vyuo vikuu kulinganishwa na mwaka 2019 ambapo wanafunzi 112 walijiunga na vyuo vikuu katika kaunti ya marsabit.
Ni watahiniwa 2,013 waliufanya mtihani huo katika kaunti hii.
Hii ni kwa mujibu wa Mkurugezi wa Elimu kaunti ya Marsabit Apollo Apuko, ambaye amesema idadi hiyo imeogezeka mwaka 2020 licha ya kuwepo kwa virusi vya corona.
Akizungumza na shajara ya radio jangwani afisini mwake, Apuko amedokeza kwamba watahiniwa wawili walipata alama ya B ya kuongeza 25 B ya kusimama 58 B ya kutoa na 110 walipata alama ya C ya kuongeza.
Wanafunzi 225 walipata alama ya D- huku wengine 30 wakisajili alama ya E katika mtihani huo.
Matokeo ya wanafunzi watatu yalifutiliwa baada yao kupatikana na makosa ya udaganyifu.
Apuko amewapongeza walimu jimboni kwa juhudi za kuipa kipaumbele elimu katika kipindi kigumu ambapo shughuli za masomo ziliathirika kufuatia mlipuko wa janga la corona.