Marehemu padre Frank atajwa kama mtu mkarimu aliyependa kusaidia wasiojiweza katika jamii.
January 22, 2025
By Isaac Waihenya,
Mkugenzi katika idara ya kilimo katika kaunti ya Marsabit Julius Gitu amesema kilimo kwenye kaunti ya Marsabit kimeadhirika kwa kiwango kikubwa kutokana na mabadiliko ya tabia nchi.
Kwa mujibu wa Gitu ni kwamba hali hiyo imesababisha ukosefu wa mvua na kuchangia kwa wakulima kupata mazao duni.
Mabadiliko hayo ambayo ameyataja kusababishwa na uharibifu wa mazingira yamefanya mvua kuwa chache na kipindi cha kiangazi kuwa kirefu.
Hata hivyo Gitu amewahimiza Wakulima kuzingatia upanzi wa mimea inayonawiri kwa muda mfupi ili kujizuia dhidi ya janga la jaa.
Ametaja uwepo wa hoja ya kuzingatia mimea inayonawiri katika maeneo kame.