Jimbo katoliki la Marsabit laadhimisha miaka 60 ya kueneza Injili.
November 23, 2024
By Waihenya Isaac,
Wakaazi mjini Marsabit wameandaa maandamano ya Amani kulalamikia ukosefu wa maji kwa muda wa wiki mbili sasa.
Wakaazi hao waliojawa na ghadhabu waliandamana hadi katika afisi ya idara ya maji mjini kuwasilisha malalamishi yao.
Wametaja kuwa imekuwa vigumu kwao kuendelea na maisha yao ya kawaida baada ya kukosekana kwa bidhaa hiyo muhimu huku wakizitaka idara husika kutatua tatizo lililopo.
Aidha wakaazi hao wameitaka serekali ya kaunti kuwajibika na kuhakikisha kuwa kero la ukosefu wa maji sawa na lile la ukosefu wa usalama jimboni linatatuliwa.
Mkurugenzi katika idara ya maji kaunti ya Marsabit Ndenge Fayo ametaja kuwa ukosefu wa maji jimboni unatokana na ukosefu wa mvua katika kaunti hii katika kipindi kirefu.
Amewataka wananchi kuwa na subira huku tatizo la ukosefu wa bili ya Stima likisuluhishwa.