County Updates, Diocese of Marsabit, Local Bulletins

Waakazi Wa Kaunti Ya Marsabit Watoa Kauli Yao Kuhusiana Na Semi Za Walala Hoi Na Walala Hai Yaani Hustlers Na Dynasties.

Picha;Hisani

By Jillo Dida,

Siku moja baada ya tume ya uwiano na utangamano kuonya dhidi ya Mjadala wa walala hoi na walala hai yaani hustlers na dynasties kwa madai kuwa inakosanisha wakenya baadhi ya wakaazi tuliozungumza nao  hapa marsabit wamedai kuwa Kenya iteendelea kugawanyika Zaidi kwenye msingi wa maskini na matajiri.

Gumzo hilo pia linaonekana kuadhiri zaidi sehemu za mashinani katika sekta tofauti tofauti.

Edward Kimathi ni mkaazi na mfanyibeishara hapa jimboni Marsabit.

“Sisi wenyewe ni kama tumechanganyikiwa juu ukiangalia pande hii unaona Uhuru pande hii na watu wake na pande hii ingine Ruto na watu wake, sisi watu wa mkono chini tunashindwa ni wapi tutaegemea, as tunaendelea sioni mambo ikienda sawa,” alisema Edward Kimathi.

Kwa upande wake Cathrine Kaweri ambaye pia ni mwenyekiti wafanyibeishara ndogo ndogo hapa jimboni ameteta kuwa biashara yao imeendelea kudunishwa kwa msingi wa hustle.

Picha;Hisani

Aidha NCIC hapo jana iliwataka wanahabari kutoeneza filosofia ya mjadala huo kote nchin. Hapa jimboni pia wametakiwa kutochangia uhasama kwenye swala nzima la walala hai na walala hoi.

Haya yamejiri huku Tume Ya Uwiano Na Utengamano Nchini NCIC pia ikionya Wanasiasa dhidi Ya Kutumia matamshi ya walala hoi na walala hai kwenye kampeni zao.

 

 

Subscribe to eNewsletter