Jimbo katoliki la Marsabit laadhimisha miaka 60 ya kueneza Injili.
November 23, 2024
Picha;Hisani
By Samuel Kosgei,
HUKU utovu wa nidhamu shuleni ukizidi kushuhudiwa na shule kadhaa kuteketezwa na wanafunzi nchini, wito wa suluhu kupatikana unazidi kutolewa na viongozi wa kidini. Kufikia sasa shule zaidi ya 10 zimeteketezwa na wanafunzi kote nchini.
Akizungumza na shajara ya radio jangwani, askofu wa kanisa la ACK jimboni Marsabit Wario Qampicha amesema kuwa ni jambo la kufisha moyo kuona vijana wakichoma mabweni na shule kitu anachosema kuwa wanaharibu maisha yao ya siku zijazo.
Anasema ni suala nzito ambalo linahitaji kushughulikiwa na wakashikadau wote bila kuachia uongozi wa shule pekee yake.
Askofu Qampicha aidha amelaumu wanasiasa anaosema kuwa ni vilelezo mbaya kwa vijana ikizingatiwa kuwa wao wenyewe wanafanya vitendo visivyo vya kuigwa hadharani.
Kwa upande wake Imam wa msikiti wa Jamia mjini Marsabit Sheik Mohamed Noor naye anayesema ingekuwa vyema iwapo walimu watazungumza na wanafunzi kujua ni wapi tatizo lipo ili kupata suluhu kabla ya kulaumu wanafunzi mwanzo.
Hata hivyo hajawasaza wanafunzi wakorofi akisema kuwa wanafaa kuadhibiwa na hata kunyimwa vyeti vya tabia njema kama walivyopendekeza idara ya polisi. Kauli ya adhabu imekaririwa pia na askofu Qampicha anayesema kuwa anaunga mkono iwapo adhabu ya viboko itarejeshwa.