Padre Francisco (Frank) Terragni kupumzishwa hiyo kesho Alhamisi….
January 22, 2025
Na Waihenya Isaac,
Viongozi ambao hawashabikii swala la Amani katika kaunti ya Marsabit hawafai kuchaguliwa kwa vyovyote vile.
Hayo ni kwa mujibu wa Askofu wa kanisa la Kiangilikana katika kaunti ya Marsabit Daniel Qampicha.
Akizungumzasiku ya jumapili katika kaunti ya Marsabit wakti wa maadhimisho ya miaka 10 tangu kuasisiwa kwa Dayosisi ya Marsabit, Askofu Qampicha amewalaumu viongoozi wa kaunti hii kwa kutoweka mifano miema kwa wananchi ili kusitisha kero la ukosefu wa usalama.
Alikariri kuwa ni vyema viongozi wa kaunti ya Marsabit na kaskazini mwa nchi kusita kunyoosheana lawama wakti panapotokea mizozo na kuwa katika mstari wa mbele kuhubiri umoja.
Kiongozi huyo wa kidini aliwataka viongozi hao kuwajibikia usalama kikamilifu na kuhubiri Amani katika mikutano yao.
Askofu Qampicha alilitaja swala la Amani kuwa jukumu la kila mmoja huku akirai serekali kuu, idara ya usalama ikiongozwa na waziri Fred Matiangi na Rais Uhuru Kenyatta kutokaa kimywa wakti wananchi wa Marsabit wana malizana wenyenye kwa wenyewe na kuwataka kuingilia kati ili kukomenya unyama huo.
Kuhusiana na swala la bodaboda kupigwa marufuku mjini Marsabit Askofu Qampicha aliitaka idara ya usalama jimboni kurejelea swala hilo upya huku akiwarai vijana kutotumika vibaya na wanasiasa haswa kipindi hichi cha kampeni.