JAMII YA MARSABIT YATAKIWA KUJITOKEZA KUPIMWA UGONJWA WA MENINGITIS ILI KUPATA MATIBABU MAPEMA.
November 15, 2024
By Samson Guyo,
Shuguli ya kuwagawia wafanyibiashara nafasi haswa walio adhirika baada ya ubomozi uliofanyika kabla ya ujenzi wa soko jipya la Marsabit imerejelewa hii leo.
Kulingana na mwenyekiti wa manispaa ya mji wa Marsabit Roba Sereka, ni kuwa shughuli hiyo iliweza kufanywa kwa usawa huku wakipokea malalamishi ambayo wameahidi kufuatilia kwa kina.
Vilevile Manispaa ya mji wa Marsabit imetaja kuwa ingali inaendelea na shughuli ya kuwapa wafanyibiashara nafasi zilizosalia.
Roba ametaja kuwa hadi kufikia sasa mfumo wa kugawa sehemu hizo za biashara umefuata utaratibu unaofaa kwani idadi ya wanaolalamika kuachwa nje ya zoezi hilo imepungua kwa kiasi kikubwa.
Mwishoni mwa mwezi jana,soko jipya la Marsabit lilifungua milango yake kwa wafanyibiashara baada ya kufunguliwa rasmi na Gavana wa Marsabit Mohamud Ali mapema mwaka huu.