Jimbo katoliki la Marsabit laadhimisha miaka 60 ya kueneza Injili.
November 23, 2024
By Guyo Godana.
NA Guyo Godana
Wakaazi wa eneo la Toricha katika wadi ya Maikona, wamelalamikia kusahaulika n ahata kutelekezwa na serikali ya kaunti ya Marsabit.
Wenyeji hao wakiszungumza na Radio Jangwani wanasema kwamba zahanati ilijengwa katika eneo hilo miaka mitano iliyopita ila kufikia sasa hawajaona matunda yoyote ya zahanati hiyo.
Wanasema kuwa sasa wanalazimika kutembea kilomita takriban 60 kutoka eneo hilo hadi Maikona jkutafuta huduma ya matibabu licha ya kuwa na jingo lililolengwa kuwa zahanati.
Aidha wameifichulia Jangwani kuwa serikali ya kaunti ya Marsabit ilimwajiri muuguzi kuhudumu katika zahanati hiyo ila tangu kuajiriwa kwake hajawahi kanyaga katika eneo hilo.
Wenyeji ambao wamegubikwa na hasira kwa kukosa huduma ya afya wamekiri kuwa kinamama na watoto wadogo wanapougua wanapelekwa hadi eneo la maikona kupata matibabu.
Aidha Chifu wa Eneo hilo Ibrae Jaldesa akiongea na Shajara ya jangwani kwa njia simu, ameweka wazi kuwa ni ukweli zahanati hiyo imekuwa na muuguzi licha yake kutokanyanga eneo hilo hadi sasa.
Chifu huyo ameshikilia dawa zilizotengewa zahanati hiyo pamoja na muuguzi zimekwama Maikona licha ya waakazi hao kung’ang’ana na hali tete ya maisha.