Marehemu padre Frank atajwa kama mtu mkarimu aliyependa kusaidia wasiojiweza katika jamii.
January 22, 2025
Na Waihenya Isaac,
Serikali kwa ukishirikiano na mashirika tofauti nchini imefaulu kukabili nzige wa Jangwani ambao wamekuwa wakiwahangaisha wakulima na kuharibu mimea mashambani kwenye maeneo mbali mbali hapa nchini.
Kulingana na waziri wa ugatuzi Eugine Wamalwa ni kuwa serikali ikishirikiana na shirika la umoja wa mataifa la chakula na kilimo FAO,imehakikisha kwamba nzige hao wanaangamizwa.
Aidha Wamalwa ameongezea kwamba serikali iko macho na iko tatari kukabiliana na wimbi jengine la nzige iwapo litachipuka.
Mwaka jana wakulima pamoja wafugaji walikadiria hasara kubwa baada ya nzige hao kuvamia mimea pamoja na malisho ya mifugo katika maeneo mengi humu nchini.