County Updates, Local Bulletins

Serekali yatenga Shillingi billioni 2.227 za awamu ya kwanza ya ujenzi wa Barabara kuu ya Marsabit-Shegel

Picha;Hisani

By Samson Guyo & Grace Gumato

Serekali imetenga Shillingi billioni 2.227 za awamu ya kwanza ili kujenga Barabara kuu ya Marsabit-Shegel ikiwa ni mpango wa kutengeza barabara kuu kutoka Marsabit kuelekea Northhorr.

Akizungumza na shajara ya radio jangwani mhandisi mkuu wa mradi huo Joel wairua ameelezea kuwa awamu hiyo ya kwanza inalenga kuinua hadhi ya barabara hiyo ambayo  kufikia  sasa asilimia 6 imekamilika.

Aidha Wairua ameelezea changamoto wanazokumbana nazo katika ujenzi wa barabara hiyo ikiwemo vijana kufunga barabara kwa madai ya kutopewa ajira.

Wairua amewarai wakaazi  kutopinga mradi wa ujenzi wa barabara kwani ni kwa manufaa ya wenyeji huku akitaja kuwa  vijana wasio na ajira  na wana ujuzi watapata nafasi za kazi katika mradi huo.  

Subscribe to eNewsletter