Marehemu padre Frank atajwa kama mtu mkarimu aliyependa kusaidia wasiojiweza katika jamii.
January 22, 2025
By Waihenya & Qabale,
Pana haki ya kuwa na usawa wakti wa ugavi wa rasilimali za umma kwa watu katika kaunti ya Marsabit.
Kwa mujibu wa mwenyekiti wa kamati ya bajeti katika kaunti ya Marsabit Daud Tomasop ambaye pia ni mwakilishi wadi ya Korr/Gurnet ni kuwa serekali ya kaunti haijakuwa ikitoa chakula cha msaada kwa usawa hususan kwa watu walioadhirika.
Akizungumza hii leo wakti wa uzinduzi kwa chakula cha msaada kwa wananchi walioadhirika na baa njaa katika kaunti ya Marsabit, mwakilishi wadi huyo ametaja kuwa serikali ya kaunti ina fedha za kutosha kuwapa chakula cha msaada wananchi wote walioadhirika.
Kauli yake imeshambikiwa na MCA wa wadi ya Sagate Jaldesa Sora Katelo aliyetaja hoja ya kuhakikisha kuwa chakula hicho kimefikia walengwa.
Nae afisa wa kudhibiti majanga katika mamlaka ya kukabiliana na Majanga NDMA tawi la Marsabit Jacob Letesiro ametaja kuwa mamlaka hiyo inazidi kushirikiana na washika dau wengine ili kuwasaidi wananchi walioadhirika na ukame hapa jimboni.