Idara ya jinsia kaunti ya Marsabit yalaani kisa cha mauaji ya watoto wawili mapacha katika eneo la Dololo,North Horr.
January 23, 2025
By Mark Dida,
Polisi wa kenya kwa ushirikiano na wale wa nchi jirani ya Ethiopia wanaendelea na uchunguzi wa kisa ambapo mhudumu wa boda boda aliuwawa na pikipiki yake kuchukuliwa katika mtaa wa Harosa lokesheni ya Butiye huko mjni Moyale jana jioni.
Kulingana na naibu kamishna wa moyale William ole kakimoni ni kuwa kwa sasa vyombo vya usalama kutoka nchi zote mbili vinaedelea na oparesheni ya kusaka waliotekeleza mauaji ya mwanabodaboda huyo huku mwili wa marehemu ukirejeshwa nchni Ethiopia.
Aidha Kakimoni amesema kuwa haijabainika kiini hasa cha mauaji ya jamaa huyo huku polisi wakidai huenda ni kisa cha wizi wa kimabavu.
Hata hivyo kakimoni ametoa wito kwa wahudumu wa boda boda wa eneo bunge la Moyale hasa mjini Moyale kuwa makini wanapoendelea na shughuli zao za kila siku kusaka riziki.
Vile vile, amewarai kuwa watulivu wakati uchunguzi ukiendelea.
Kwa mujibu wa kakimoni licha ya kisa hicho kuzua hofu kwa wenyeji wa mji wa Moyale, usalama wa mji huo umeimarishwa huku shuguli zote zikiendela kama kawaida.