County Updates, Diocese of Marsabit, Local Bulletins

Mwakilishi Wa Wadi Ya Uran Eneo Bunge La Moyale Kaunti Ya Marsabit, Halkano Konso Akamatwa Na Makachero Wa DCI Hii Leo Asubuhi Mjini Marsabit .

Mwakilishi Wa Wadi Ya Uran Halkano Konso Akiwa Katika Kituo Cha Polisi Cha Marsabit, Kabla Ya Kukamatwa.
Picha;Hisani

By Jillo Dida ,

Mwakilishi wadi ya Uran eneo bunge la Moyale kaunti ya Marsabit, Halkano Konso amejiwasilisha ktk afisi za makachero wa DCI mjini Marsabit leo asubuhi.

Duru inaarifu kuwa Halkano alisafirishwa baada ya kumaliza kuandikisha taarifa hadi eneo ambalo halijajulikana ambapo pia wanahabari walizuiliwa kuzungumza naye.

Inaarifiwa kuwa huenda Konso amesafirishwa hadi jijini Nairobi kwa mahojiano Zaidi.

Maafisa wa idara hiyo walikuwa wanamsaka Konso akihusishwa na kisa cha siku ya Jumamosi ambapo gari moja la serikali ya kaunti lilinaswa na maafisa wa kushika doria katika mpaka wa Turbi na Sololo.

Kwa mujibu wa idara ya usalama hapo jana, bunduki moja aina ya Ak 47 na risasi zilipatikana zikiwa na watu wanne waliokuwa wakisafiria kwenye gari hilo.

Mwakilishi Wa Wadi Ya Uran Halkano Konso Akiwa Katika Kituo Cha Polisi Cha Marsabit, Kabla Ya Kukamatwa.
Picha;Hisani

Konso, anayedaiwa kuwa mmoja wa wahusika wakuu wa sakata hiyo, anasemekana kuingia mafichoni baada ya kisa hicho kutokea na alitakiwa ajisalimishe la sivyo atangazwe kuwa mtu hatari aliyejihami kwa silaha na kuhusika katika visa vya ukosefu wa usalama katika Kaunti ya Marsabit.

Idara ya DCI imesema washukiwa hao wanne, miongoni mwao maafisa wawili wa serikali ya kaunti, wanashukiwa kuwasambazia silaha na chakula majambazi kwenye msitu wa Funa Qumbi.

Subscribe to eNewsletter