County Updates, Local Bulletins

Mtu mmoja ajeruhiwa baada ya mzozo kati ya jamii mbili kuzuka Jumatano asubuhi katika eneo la Arapal.

Kamishna Wa Kaunti Ya Marsabit Paul Rotich.
Picha;Hisani

Na Waihenya Isaac,

Mtu mmoja alijeruhiwa wakti mzozo kati ya jamii mbili ulipozuka hii leo asubuhi katika eneo la Arapal wadi ya Loiyangalani kaunti ya Marsabit.

Akidhibitisha kisa hicho kamishina wa kaunti ya Marsabit Paul Rotich ametaja kuwa mzozo ulizuka baina ya jamii mbili kuhusiana na eneo la malisho japo swala hilo lilitulia baadae.

Rotich amearifu kuwa maafisa wa usalama walitumwa katika eneo hilo mara moja ili kuokoa jahazi.

Katika kisa kingine eneo la Kargi,wafugaji katika eneo hilo wanahesabu hasara baada ya idadi ya mifugo wasiojulikana kuibiwa usiku wa kuamkia leo.

Kamishina Rotich ametoa wito kwa wananchi jimboni kudumisha Amani na kusitisha vitendo vya kinyama.

Aidha mkuu huyo wa usalama ametaja kuwa uchunguzi kuhusiana na kisa cha maujai kilichotokea wiki jana katika eneo la Bank Quarters bado unaendelea.

Leave a Comment

Your email address will not be published.

Subscribe to eNewsletter