Marehemu padre Frank atajwa kama mtu mkarimu aliyependa kusaidia wasiojiweza katika jamii.
January 22, 2025
By Waihenya Isaac,
Mtoto aliyeokolewa na maafisa wa polisi katika shimo la choo,jumamosi wiki jana yuko salama na anaendelea vyema.
Kwa mujibu wa afisa mkuu katika hospitali ya rufaa ya Marsabit Liban Wako ni kwamba mtoto huyo wa wiki moja aliokolewa na maafisa wa polisi Katika choo kimoja hapa mjini na baadae kumwasilisha hospitalini kwa ajili ya Matibabu.
Ameleza kuwa mtoto huyo aliye na uzani wa kilo 3.3 huenda alizaliwa katika mojawepo ya hospitali hapa mjini Marsabit kabla ya mzazi wake kumtupa katika shimo la choo kwani aniakipini kwenye kitovu kinawekwa mtoto anapozaliwa hospitalini.
Liban amesema kuwa mtoto huyo atasalia chini ya ungalizi wa madaktari hospitalini huku shughuli za kumkabidhi kwa familia moja iliyojitolea kumlea zikiendelea kupitia idara ya watoto jimboni.