Idara ya maji Marsabit yaahidi kukabiliana na utata unaozunguka kero la maji
January 20, 2025
By Mark Dida,
Mshukiwa wa wizi wa mifugo aliyenaswa na maafisa wa polisi siku ya ijumaa kufuatia makabiliano na wahalifu lokesheni ya Mata Arba eneo la Saku hakufikishwa mahakamani hii leo ilivyotarajiwa.
Kulingana na OCPD wa Marsabit Central Johnston Wachira ni kuwa idara ya Upelelezi DCI imeomba mahakama siku zaidi ya kufanya uchunguzi baada ya simu ya mshukiwa kupatikana.
Aidha Wachira ametoa wito kwa wakaazi wa jimbo hili kupiga ripoti kwa maafisa wa usalama kuhusu wizi wa mifugo na kusaidia polisi wakti oparesheni inapoendelea.
Hata hivyo mshukiwa huyo angali kizuizini na anatarajiwa kufikishwa mahakamani pindi uchunguzi utakapokamilika.
Mshukiwa alitiwa mbaraoni huku maafisa wa polisi wakifanikiwa kuwarejesha zaidi ya mifugo 29 walioibiwa Alhamisi jioni katika eneo la Mata Arba badaa ya makabiliano makali na majangili wa wizi wa mifugo.