County Updates, Local Bulletins

Mna Jukumu la kuwalea na kuwalinda watoto wenu, afisa wa watoto kaunti ya Marsabit awaambi wazazi.

Picha;Hisani

By Waihenya Isaac,

Ni wajibu wa kila mmoja kuhakikisha kuwa watoto wanapata haki zao na pia wanalindwa kikamilifu.
Haya ni Kwa mujibu wa afisa wa watoto katika kaunti Marsabit Kenneth Mutuma.
Mutuma amesema kuwa sio jukumu la maafisa wa watoto kuwalinda watoto bali ni jukumu la jamii kuhakikisha kuwa kila mtoto yu salama na anapata haki zake za kimsingi.
Mutuma ameitaja jamii kama mshikadau mkuu katika kulinda haki za watoto bila kujali jinsia yao.
Aidha Mutuma amesema kuwa jumla ya visa 344 vya dhulma za watoto vililipotiwa katika mwaka wa 2020/2021.
Kati ya visa hivyo, visa 11 vya dhulma za kimapenzi kwa watoto vilirekodiwa huku zaida ya watoto 150 wakinyimwa haki ya elimu.
Idadi ya visa vya wazazi kutelekeza majukumu yao katika familia ikitajwa kuongezeka.
Mutuma ameirai jamii pia kukomesha mila potuvu kama vile ukeketaji na ndoa za mapema ambazo ametaja kuwa zinamwadhiri mtoto wa kike jimboni.

Subscribe to eNewsletter