Jimbo katoliki la Marsabit laadhimisha miaka 60 ya kueneza Injili.
November 23, 2024
By Samuel Kosgei,
Mbunge Wa North Horr Chachu Ganya Amelaani Vikali Visa Vya Mauaji, Uvamizi Na Wizi Wa Mifugo Uliofanyika Wiki Jana Katika Eneo La Halakha Yahya Na Turbi Ambapo Watu Wawili Waliuawa Kwenye Matukio Tofauti Huku Mifugo Zaidi Ya 300 Wakiibiwa.
Akizungumza Na Shajara Ya Jangwani, Ganya Ameonekana Kuunyosha Kidole Cha Lawama Kwa Viongozi Wa Kaunti Akidai Kuwa Uongozi Huo Unaegemea Upande Mmoja. Anasema Wachochezi Na Wafadhili Wa Uovu Unaoshuhudiwa Kaunti Ya Marsabit Wanafahamika Vyema Na Serikali Ila Hatua Mwafaka Haijawahi Kuchukuliwa Miaka Nenda Miaka Rudi.
Wakti Uo Huo Anadai Kuna Udhaifu Katika Uongozi Wa Kaunti Suala Analosema Linachangia Pakubwa Kuyumbayumba Kwa Hali Ya Usalama Jimboni.
Hapo Jumatatu Wakihutubu Jijini Nairobi Baadhi Ya Viongozi Wa Jimbo Hili Walilaani Pia Mashambulizi Hayo Na Kutaka Serikali Ifanye Juhudi Kurudisha Mifugo Walioibiwa Katika Eneo La Halakha Yahya. Dido Raso Na Qalicha Gufu Ni Wabunge Saku Na Moyale Mtawalia.
Mwakilishi Wa Kina Mama Wa Isiolo Rehema Jaldesa Alidai Kuwa Mavamizi Ambayo Yanafanyika Kaunti Za Isiolo Na Marsabit Yana Uhusiano Kwani Yalifanyika Kwa Kipindi Sawa. Analaumu Uchochezi Wa Viongozi Akipuuza Kuwa Ni Mvutano Kwa Ajili Ya Raslimali.
Gavana Mohamud Ali Pia Alitoa Wito Kwa Waziri Wa Usalama Fred Matiangi Kushughulikia Usalama Wa Jimbo Lake Huku Akimshutumu Waziri Wa Hazina Ya Kitaifa Balozi Ukur Yatani.
Mbunge Chachu Ganya Naye Anadai Kuwa Idara Ya Usalama Imelala Kazini Kwa Kutowachukulia Hatua Washukiwa Na Wahalifu Hao Licha Ya Kuwa Wanajulikana.