Padre Francisco (Frank) Terragni kupumzishwa hiyo kesho Alhamisi….
January 22, 2025
Na Waihenya Isaac,
Maseneta wamemtaka waziri wa elimu George Magoha pamoja na wakuu wa chama cha shule za upili KESHA kufika mbele yake kutoa maelezo kuhusiana na kukithiri kwa visa vya uteketezaji wa majengo ya shule.
Maseneta hao aidha wamelalamikia utovu wa nidhamu ya wanafunzi miongoni mwa wanafunzi vilevile kipindi kirefu cha masomo ili kufidia muda uliopotezwa wakti shule zilikuwa zimefungwa kutokana na janga la korona kuwa miongoni mwa sababu zinazochangia kwa ongezeko la uteketezaji wa majengo shuleni.
Haya yanajiri huku shule ya Shule ya upili ya wasichana ya Moi hapa jimboni kufungwa kwa muda usiojulikana baada ya bweni moja shuleni humo kuteketea usiku wa kuamkia leo.
Visa vya utovu wa nidhamu katika shule mbali mbali nchi vimeongezeka tangu wanafunzi kurejea shuleni kutoka rikizo ndefu ya korona.