Jimbo katoliki la Marsabit laadhimisha miaka 60 ya kueneza Injili.
November 23, 2024
By Samuel Kosgei,
Askofu wa Jimbo Katoliki La Marsabit Peter Kihara amesema kuwa kipindi hiki wakatoliki wote dunia wanapoanza kipindi cha kwaresma ni wakti mwafaka wa kufanya toba na kuzungumza na Mungu.
Akihubiri katika kanisa Kuu la Parokia ya Maria Consolata mjini Marsabit, Kihara amewataka wakristo kutumia wakti huu kujiangalia, kujitakasa na kukiri makosa zao.
Anasema kuwa huu ndio wakti mzuri kwa wakristu wote kwenda mbele za Mungu kujiombea sawia na nchi nzima.
Wakti uo huo Askofu Kihara amewataka wakrsitu wote kufanya mfugo wa kweli huku akiomba kila mmoja atumie msimu huu wa kwaresma kuvumiliana na kudhibiti ndimi anazozitaja Kama chanzo cha dhambi na pia uchochezi.
Kwaresma ni kipindi ambapo wakristu hujiandaa kabla ya siku kuu ya pasaka. Ni kipindi cha mfungo kinachoanza Jumatano ya majivu na kukamiliki siku ya Jumapili ya matawi.
Msimu wote huo wakrsitu haswa wakatoliki hufunga kwa siku 40, hufanya toba ama kutubu, kujikana na kuweka nidhamu ya kiroho.