Jimbo katoliki la Marsabit laadhimisha miaka 60 ya kueneza Injili.
November 23, 2024
By Adano Sharawe,
Wazazi na wanafunzi kutoka kaunti ndogo ya Laisamis wanasherehekea matokeo bora ya mtihani wa KCPE mwaka huu, wengi wao wakiwa wamepata alama 300 na zaidi.
Hata hivyo, walielezea masikitiko yao ya kushuka kwa matokeo hayo kulinganisha na mwaka 2019.
Kulingana na mzazi Edward Delea, janga la corona liliwakoroga wanafunzi wao ila walijikaza kufa kupona.
Edward ambaye ni daktari ni babake mwanafunzi bora katika shule ya msingi ya Laisamis Valgelista Kulmise Delea ambaye alipata alama 365.
Kulingana na mzazi huyo ni kuwa changamoto za kuhamahama kwa wafugaji pia zimechangia watoto wengi kupata matokeo ambayo hawakutarajia.
Amesema wakati huu ambapo shule zimefungwa wazazi wanapaswa kujukumika kama inavyopaswa kwa kufuatilia maendeleo ya elimu ya wanao.
Kwa upande wake Delea amesema kwamba kupitia ushirikiano mwema wa walimu pamoja na wazazi na kuzidi kuwa na nidhamu kumemsaidia kufanya vyema katika mitihani hiyo.
Delea amesema ana ndoto ya kuwa wakili.
Naye mamake Delea, Francisca Delea ambaye ni mwalimu wa shule ya upili amewataka wazazi kulea vyema watoto wa kike ili kuwasaidia kumaliza masomo yao na kuwa watu wa manufaa katika jamii.
Waziri wa elimu Profesa George Magoha akitangaza matokeo hayo alisema wanafunzi wote waliofanya mtihani huo watajiunga na shule za upili.
Shilingi bilioni nane kulingana na waziri Magoha, zimetengwa ili kuboresha miundo mbinu katika shule za upili kwenye kaunti ndogo 110 kote nchini ili kuwezesha wanafunzi wote waliofanya mtihani wa KCPE kujiunga na shule za upili.
Aidha Mwafunzi katika kaunti ndogo ya Laisamis ni Nashipai Baru Chana kutoka shule ya msingi ya Tereem katika eneo la Korr aliyejizolea alama 382.