County Updates, Local Bulletins

Kaunti ya Marsabit imetajwa kuwa miongoni mwa kaunti ambazo zinashuhudia visa vingi vya mimba za mapema.

Picha; Hisani

Na Silvio Nangori,

Kaunti ya MARSABIT imetajwa kuwa miongoni mwa kaunti ambazo zinashuhudia visa vingi vya mimba za mapema.

Kaunti zingine katika maeneo ya kaskazini mashariki mwa Kenya -Embu, Kitui na Machakos zimetajwa pia kuathirika.

Kaunti ya Nairobi imetajwa kuongoza nchini kwa visa vingi Zaidi mwaka huu.

Haya ni kwa mujibu ya ripoti iliyotolewa hii leo na Baraza la kitaifa la kudhibiti ugonjwa wa ukimwi (NACC).

Takwimu zinaonyesha kwamba wasichana 2,379 kati ya miaka 10 hadi 14 walitungwa mimba za mapema miezi 10 zilizopita.

Kaunti zingine ni kama Kajiado (1,496), Mandera (1,370) na Bomet (1,041).

Kwanzia mwezi wa januari hadi October 2021 kaunti tisa Trans Nzoia, Vihiga, Tharaka Nithi, Nandi, Lamu, Kwale, Kericho, Narok na Muranga zilionyesha kupungua kwa idadi ya visa.

Ikumbukwe kwamba mwaka uliopita baada ya ujio wa virusi vya Korona visa vya mimba za mapema vilitajwa kuongezeka maradufu katika kipindi ambacho wanafunzi walisalia nyumbani.

 

Subscribe to eNewsletter