Understanding Elavil: Uses, Benefits, and Safety
December 26, 2024
By Mark Dida,
Kaunti ya marsabit haijasajili visa yoyote vya maambukizi ya corona chini ya saa 24 zilizopita, ikisajili visa 147 tangu mlipuko wa virusi vya corona kuripotiwa nchini Machi mwaka uliopita.
Hii ni baada ya sampuli 1164 kupimwa, mgonjwa mmoja aliaga dunia kutokana na makali ya virusi hivyo katika hosipitali ya rufaa ya Marsabit.
Hii ni kwa mujibu wa mkurugenzi mkuu wa wizara ya afya kaunti ya Marsabit ADANO KOCHI.
Aidha kochi amebaini kuwa kati ya wagonjwa hao 147, 138 ni wakenya, WaEthiopia 9 na MuEritrea mmoja.
Wakati uo huo, Kochi amewatahadharisha wakazi wa kaunti hiI dhidi ya kukiuka masharti yaliyowekwa kukabiliana na janga la Corona akiongeza kuwa kuna uwezekano wa wimbi jipya la mlipuko wa virusi hivyo kutokea kama ilivyo shuhudiwa katika mataifa tofauti ulimwenguni.
Kochi amesema kuwa wengi wa wakazi wamegeukia mienendo ya awali na kukiuka kabisa masharti yaliyowekwa na wizara ya afya ya kudhibiti kusambaa kwa virusi vya corona.