Padre Francisco (Frank) Terragni kupumzishwa hiyo kesho Alhamisi….
January 22, 2025
Na Waihenya Isaac,
Idara ya polisi nchini imetoa onyo kwa viongozi wa kisiasa wanaowatumia vibaya vijana kuleta virugu miongoni mwa jamii wakati huu tunapokaribia uchaguzi mkuu mwaka ujao.
Akizungumza na waandishi wa habari inspekta jenerali wa polisi Hillary Mutyambai amesema kuwa idara ya polisi iko macho na itatumia mbinu zozote zile ili kuwanasa wanasiasa hao na kuwachukulia hatua za kisheria
Mkuu huyo wa polisi amewahakikishia wananchi usalama wa kutosha kipindi hichi cha kampeni huku akiwataka kuishi na amani miongoni mwao akidai kuwa idara ya usalama imejipanga vilivyo katika kuhakisha kuwa amani inadumishwa.
Amekariri kuwa idara hiyo itatumia baadhi ya vijana waliojisalimisha na kujirekebisha tabia kutoka katika vikundu vya uhalifu katika maeneo mbalimbali nchini kuwanasa vijana ambao bado wamo katika magenge ya uhalifu.