Marehemu padre Frank atajwa kama mtu mkarimu aliyependa kusaidia wasiojiweza katika jamii.
January 22, 2025
By Mark Dida,
Idadi ya wanao ugua ugonjwa wa saratani ya mlango wa uzazi huenda ikaongezeka katika kaunti ya Marsabit kutokana na wanawake kupuuza zoezi la kupimwa mapema.
Kwa mujibu wa mhudumu wa afya anayesimama kitengo cha kuchunguza saratani katika hospitali ya rufaa ya Marsabit Rose Mary Boke ni kuwa hadi kufika sasa kaunti ya marsabit imerekodi visa 144 vya akina mama wanaouguwa ugonjwa wa saratani ya malango ya wazazi.
Visa hivyo vimenakiliwa katika kipindi cha miezi minne iliyopita, huku maeneo bunge ya Saku, Laisamis na North horr yakitajwa kuadhirika zaidi.
Boke amesema kuwa wanawake kati ya umri wa mika 25 hadi miaka 50 wamo hatarini kuambukizwa ugonjwa wa saratani ya malango wa uzazi.
Aidha Boke ameeleza kuwa kitengo hicho kina wahudumu wa afya waliopata mafunzo ya kutumia maishini aina ya chemotherapy kuchoma seli za kuambukiza ugonjwa wa saratani.
Boke vilevile ameeleza kuwa chanzo kikuu cha ugonjwa wa saratani ni kushiriki kwenye tendo la ndoa na watu zaidi ya wawili huku akiwataka wananchi kumakinika.
Ametoa wito kwa akina mama kujitokeza na kufanyiwa uchunguzi wa mara kwa mara huku akisema kuwa kugunduliwa mapema kwa ugonjwa huo kuna weza kumsaidia mgonjwa kutibiwa na kupona.